Saturday, March 20, 2010

Kweli nimeamini Burudani ni Nyumbani Mh Mohammed Dewji Azidiwa

Ngoja nijaribu sijui nitachekesha
Kweli kila mtu na kazi yake, sijui niluke chini.
Mh Mohammed Dewji alishindwa kujizuia baada ya kupagawishwa na bendi ya Twanga Pepeta, cha kushangaza aliendanao sambamba na kuwaachia maswali wapenzi na wadau wa muziki kwamba amejifunzia wapi? lakini baada ya mda akawajibu kuwa ni mfuatiliaji mzuri sana wa kipindi cha Burudani ni Nyumbani kinachorushwa kupitia Tbc1.

Akudo Impact yaipua vibayo viwili, Heshima kwa wanandoa iliyotungwa na Cristian Bella na nyingine Ubinafsi iliyotungwa na Tarsis Masela

Toto ze Bingwa (Rapa wa Akudo Impact)
Akudo Impact wakiwa kazini

Rais wa Akudo Impact Cristian Bella a.k.a Obama,. kwa taarifa tu ni kwamba Bell amefiwa na kaka yake na anatalajia kuondoka kwenda Congo baada ya kumaliza tu show za pasaka. Burudani ni Nyumbani inampa pole sana na inamtakia safari njema.


SIO KUIMBA TU NA HUKU NIMO!


Mwanamuziki Khalid Mohamed a.k.a TID, akiwa mazoezini na inasemekana ni desturi yake kila siku kufanya mazoezi. INAPENDEZA

Salam ni muhimu


Mwanamuziki wa Fm Academia Patcho Mwamba (Tajili) akiwasalimia wanamuziki wa Twanga pepeta na wapenzi kwa ujumla katika ukumbi wa Club Bilcanas, Twanga hutumbuiza kila jumatano.

Musa na Lisa wakiwasili kunduchi beach hotel kwenye semina ya siku 2 ya Kili Music Awards

Kutoka kushoto ni Dina Marios, Lisa na Musa

Unawafahamu hawa? ni baadhi ya watangazaji maarufu wa kike wakiwa katika picha ya pamoja, na ndio majaji wa kike pekee wa Kili Music Award

Lisa akiwa na watangazaji wenzake wakike

Mashujaa band wakifanya vitu vyao katika moja ya shoo zao wanazopiga pale mashujaa pub

Warembo wa Mashujaa band wakiwa kazini

Friday, March 19, 2010

Dogo Rama na Luiza Mbutu wakifanya vitu vyao.

Wasanii Mahiri wa Bendi ya Twanga pepeta, Luiza mbutu (Kulia) na dogo rama (mwenye jeans) wakikamua kiufundi katika moja ya show zao.

MCD mpiga tumba maarufu wa bendi ya Twanga pepeta hadi sasa ni wachache wanaolifahamu jina lake halisi...!

Sudi Mohammed a.k.a MCD

Thursday, March 18, 2010

MUSA NA LISA WALILIWA MIKOANI

Baada ya kubamba katia kipindi cha Burudani ni nyumbani,watangazaji mahili Musa na Lisa waliliwa mikoani kwa kupokea kila siku barua za mwaliko kutoka katika mikoa mbalimbali ikiwemo Tanga, Mbeya, Mtwara,Mwanza, Tabola na mengine mengi. kwa mujibu wa Musa na Lisa wamesema walikuwa wanajipanga na hivi karibuni watasema wataanza mkoa gani

DAIMOND MUSICA WAVAMIA KINONDONI

Band ya Daimond Musica baada ya kupiga shoo kabambe ya kujitambulisha kinondoni
na wadau kukubali, yaamua kung'ang'ania kwa kuamua kupiga kili ijumaa pale sterio pub pale kinondoni. sasa kazeni butu msije mkashindwa kuendelea. Burudani ni Nyumbani ipo nyuma yenu.

Wednesday, March 17, 2010

TOP BAND YAONGEZA WAWILI

Band ya top band imezidi kujipanga zaidi baada ya kuongeza nguvu kwa kuongeza
wanamuziki wawili. big up top

MUSA NA LISA WAZIDI KUNG'ARA

Watangazaji mahili wa mziki wa Dansi nnchini Musa na Lisa wanaotangaza katika
kipindi cha Burudani ni Nyumbani, wamechaguliwa kuwa katika majaji kati ya 100
walioteuliwa katika Kili Music Awrds.

MAPACHA WAJIPANGA

mapacha 3 wajipanga kwa ajili ya video yao mpya, kundi hilo linaloundwa na Jose mala, Kalala junior na Khalid chokora. wapenzi wa mapacha kaeni tayari